Sepesha Rushwa Marathon kufanyika Des.11

Sepesha Rushwa Marathon kufanyika Des.11

WAKIMBIAJI  zaidi ya 2000 wanatarajia kushiriki Sepesha Rushwa Marathon,  yanayotarajiwa kufanyika Desemba 11 mwaka huu jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa mabalozi wa sauti ya wapinga rushwa Mkoa wa Dodoma, Haruna Kitenge, alisema awamu ya kwanza wakimbiaji zaidi ya 2000 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanatarajia kushiriki.

Alisema mbio hizo ni kutekeleza kampeni ya Sepesha Rushwa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Arusha kama mikoa ya majaribio kwa miaka mitatu, mpaka ifikapo mwisho Desemba 2025.

Advertisement

Alisema mbio hizo zitahusisha wakimbiajji wa kilomita 20, kilomita 15 na kilomita tano.

Alisema kundi la  kwanza ni la wanafunzi  wa shule za msingi, sekondari na vyuo, ambao ni pamoja na mabalozi wa sauti ya wapinga rushwa.

Alisema kundi la pili ni la watumishi wa serikali na sekta binafsi, ambao ushiriki wao kwenye mbio hizo ni utekelezaji wa mkakati wa serikali dhidi ya rushwa awamu ya tatu.

Aliitaja kundi la tatu ni la wakimbiaji na wananchi  wote kwa ujumla wao.

“Usajili ulianza Septemba 16, unafanyika kupitia tovuti ya www.anticorruptionvoices.or.tz au tovuti ya washirika wao, www.eventbrain.com, ambapo katika tovuti hizo kuna ukurasa wa sepesha rushwa Marathon.

Pia gharama za kujisajili zimegawanyika katika  makundi matatu ambayo ni wanafunzi,watu wazima na V.

Ii.P, usajili.utafanyika kwa.awamu.tatu kwa gharama tofauti,” amesema.

/* */