Serengeti Girls yatinga Robo Fainali
TIMU ya soka ya taifa ya wasichana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Girls imetinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe Dunia, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Canada, mchezo wa mwisho hatua ya makundi uliofanyika Uwanja wa DY Patil mjini Mumbai, India uliomalizika muda mfupi uliopita.
Kutokana na matokeo hayo Serengeti Girls imemaliza makundi ikiwa na pointi nne, nyuma ya mabingwa watetezi Japan wenye pointi 9, baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ufaransa katika mchezo mwingine wa mwisho Kundi D uliofanyika Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru, Goa.