Serengeti hifadhi bora Afrika kwa mara ya tano
TANZANIA: Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ya Tanzania imeshinda tuzo ya hifadhi bora barani Afrika ‘African Leading National Park 2023’.
Hii inakuwa mara ya tano mfululizo kwa Serengeti kutwaa tuzo hiyo tangu 2019 hadi sasa.
–
Akitoa shukrani katika akaunti yao ya X (twitter) Ahsante kwa wote walioshiriki kupiga kura na kuiwezesha Serengeti kutwaa tuzo hiyo kwa mara nyingine, Hifadhi ya Taifa ya Tanzania (TANAPA) imeandika “Tunatoa shukrani za dhati kutoka moyoni! Asante kwa wote waliopiga kura na kufanikisha ushindi huu. Kwa pamoja, tunasherehekea ushindi mzuri wa Serengeti kwa mara tano katika Tuzo za Utalii za Dunia.
Kwa mujibu wa tovuti ya World Travel Awards, hifadhi teule katika kuwania tuzo hiyo mwaka 2023 ni pamoja na Hifadhi Kuu ya Wanyama ya Kalahari (Botswana), Hifadhi ya Kitaifa ya Etosha (Namibia), Hifadhi ya taifa ya bonde la Kidepo (Uganda), Hifadhi ya Kitaifa ya Kruger (AFRIKA KUSINI) na Hifadhi ya Kitaifa ya Masai Mara (Kenya).
–
Serengeti ni maskani ya mamia kwa maelfu ya wanyama wakiwemo Nyumbu, Pundamilia, Pofu, Simba, Duma, Fisi na Swala.