Serikali bega kwa bega na sungusungu

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amesema serikali itaendelea kulisimamia jeshi la jadi maarufu ‘sungusungu’ nakulishauri sababu linasaidia suala la ulinzi na usalama pamoja na kuhamasisha maendeleo.

Mndeme amesema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa sungusungu kwa Kanda ya Ziwa uliokutanisha mikoa mitatu ya Simiyu, Mwanza na Shinyanga nakufanyika kijiji cha Busanga wilayani Kahama.

Mndeme akiwa mshauri na mlezi wa sungusungu ndani ya mkoa huu aliwataka  sungusungu  kushiriki  kulinda miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali  maeneo yote.

Mndeme amesema  jeshi la jadi liendelee kulinda  amani iliyopo  ili isipotee na kuwaepuka watu wenye nia mbaya  na kupinga vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Mndeme amesema serikali katika mkoa wa Shinyanga imeleta jumla ya Sh trilioni 1 kutekeleza miradi ya maendeleo na uendeshaji wa sekta mbalimbali.

Habari Zifananazo

Back to top button