Serikali: Gunia ni kifungashio sio kipimo

DODOMA; Serikali imesema haitambui gunia kuwa kipimo bali ni kifungashio, Bunge limeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 6, 2023 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exhaud Kigahe, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Husna Sekiboko aliyetaka kujua kwa mujibu wa sheria serikali inatambua gunia kuwa kipimo au kifungashio.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Kigahe amesema: “Kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo “The Weights and Measures Act (Amendment) Order, G.

Advertisement

N. No. 725 of 2018”, jedwali la 10 chini ya kifungu cha (2) (b) cha jedwali hilo, ambacho kinasema mazao ya mashambani yatafungashwa kwa uzito usiozidi kilogramu 100 pamoja na kuelekeza wauzaji/wanunuzi wa mazao kutumia mizani, serikali haitambui gunia kuwa kipimo bali ni kifungashio.

“Hivyo nitoe wito kwa wadau wote kuepuka matumizi ya gunia kama kipimo kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria ya vipimo.”

3 comments

Comments are closed.