Serikali imeweka nguvu uchumi wa madini

SERIKALI imedhamiria kusimamia sheria ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanashiriki kwenye uchumi wa madini kupitia usambazaji wa bidhaa na kutoa huduma kupitia migodi nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunde jijini Dar es Salaam katika mahafali ya Chuo cha Mitambo na Teknolojia(IHET).

Amesema serikali imefanya marekebisho ya sheria kwa lengo la kusimamia ushiriki wa Watanzania kwenye uchumi wa madini, ili fursa nyingi zitokanazo na uwekezaji kwenye sekta ya madini ziweze kuwanufaisha Watanzania kupitia ajira,utoaji wa huduma na usambazaji wa bidhaa.

“Wizara ya Madini itahakikisha inasimamia kwa dhati utekelezaji wa matakwa ya sheria hii, ili kuongeza wigo wa Watanzania katika ushiriki wao kwenye sekta ya madini,”amesema Mavunde.

Amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kikiwemo chuo cha IHET, ili kuhakikisha wanaandaa Watanzania wengi zaidi kukidhi vigezo na ubora katika usambazaji wa bidhaa na utoaji wa huduma migodini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha IHET Prof. Patrick Makungu, amesema wahitimu katika mahafali hayo ni zaidi ya 2000, ambao chuo kimewazalisha tangu uanzishwaji wake na kwamba dhamira kuu ya chuo cha IHET ni kuzalisha wataalamu wenye weledi, ubora, maadili na shindani katika soko la ajira.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button