‘Serikali inaunga mkono uwekezaji uchumi wa buluu’

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amesema serikali inaunga mkono uwekezaji katika maeneo ya uchumi wa buluu ikiwemo usafirishaji wa baharini, mafuta na gesi, na bandari.

Dk Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar alipotembelewa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk Michael Anthony Battle kwa lengo la kujitambulisha.

Amesema kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kumetokana na makubaliano yaliyofanyika baada ya uchaguzi ili kutafuta njia za kutatua tofauti zilizopo ikiwa ni pamoja na kushirikiana kuendesha na kudumisha amani na utulivu nchini.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk Michael Anthony Battle ameridhishwa na utendaji wa Rais Dk Mwinyi kwa utayari wake katika sekta ya biashara na uwekezaji ikizingatiwa kuwa Marekani imelenga kuwekeza zaidi nchini na kutoa fursa za ajira.

Habari Zifananazo

Back to top button