Serikali kuanzisha akiba ya dhahabu

SERIKALI imekamilisha taratibu za kununua dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuanzisha akiba ya dhahabu hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba na kwamba kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vya kusafishia dhahabu, serikali itaendelea kuweka vivutio kwa viwanda hivyo ili vipate malighafi ya kutosha.
“Ili kukamilisha hilo serikali imepunguza mrahaba wa madini yanayouzwa kwenye viwanda hivyo kutoka asilimia sita hadi asilimia nne.
“Nafurahi kulijulisha Bunge kuwa Serikali imekamilisha taratibu za kununua dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuanzisha akiba ya dhahabu hapa nchini.“Tunataka tunapotaja akiba ya fedha za kigeni tutaje na akiba ya dhahabu tuliyonayo, hatua hii itawapatia Wachimbaji bei nzuri na kuimarisha sarafu ya nchi yetu, hii ni baada ya kupokea maelekezo ya Mh. Rais  Samia na michango ya Waheshimiwa Wabunge. “Amesema

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *