Serikali kuanzisha kituo cha zana za kilimo Geita

SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imetoa zana za kilimo ambazo ni trekta tano, pawatila 16 pamoja na viambata vyake kwa ajili ya kuwezesha kilimo cha kisasa na kuinua sekta hiyo wilayani Geita.
Hatua hiyo inalenga kuanzisha kituo cha zana za kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo wakulima watakodi zana hizo kwa gharama ndogo ili kufanikisha shughuli za kilimo katika maeneo yao.

Ofisa Manunuzi Wizara ya Kilimo Stephen Ikanga, amekabidhi zana hizo katika ofisi za halmashauri hiyo zilizopo kata ya Nzera.
SOMA: Wakulima 200 kunufaika mradi wa kilimo rafiki Geita
Ikanga amesema zana hizo ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya serikali ya awamu ya sita kuweka mazingira bora kwa makundi yote ikiwemo vijana na wanawake waweze kutumia fursa zilizopo kujiajiri na kuongeza kipato.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dk Alphonce Bagambabyaki amekiri kuwa zana hizo zitasaidia wakulima kupata huduma ya kulimiwa eneo kubwa kwa gharama nafuu.
“Tunashukuru serikali kwa kutupatia zana hizi kwani uhitaji ni mkubwa sana maana shughuli za kilimo hususani zao la mpunga zinafanyika kwa kiasi kikubwa katika maeneo yetu” amesema Dk Alphonce.
Dk Alphonce amesema zana hizo zitawasaidia wakulima wakubwa, wa kati na wadogo ambapo kwa kuzingatia jiografia pawatila zitatumika kwa maeneo ambayo trekta hazitaweza kufika na kwa wakulima wa eneo dogo.




Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com