Serikali kudhibiti mfumuko wa bei

DAR ES SALAAM: Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amesema mfumuko wa bei nchini umeendelea kudhibitiwa ambapo kwa kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka 2023 ulifikia wastani wa asilimia 3.2, kiwango ambacho kipo ndani ya lengo la kati ya asilimia 3 hadi asilimia 7.

Akizungumza katika Jukwaa la Kodi na Uwekezaji jijini Dar es Salaam leo Februari 27, 2024, Dk Mpango amebainisha kuwa katika mwaka 2023 pato la Taifa limekadiriwa kukua kwa asilimia 5.0 ikilinganishwa na asilimia 4.7 mwaka 2022 na kwamba matarajio kwa mwaka 2024 ni kufika asilimia 5.5.

Aidha, ameongeza kuwa Tanzania imeendelea kuwa kitovu cha uwekezaji na nchi yenye uchumi unaokua kwa kasi Kusini mwa Jangwa la Sahara, licha ya misukosuko ya kiuchumi na kijamii inayoendelea duniani kote.
Dk Mpango amesema pia, serikali iko mbioni kupokea ndege mpya mbili aina ya Boeing 737 9max na Boeing 787 – 8 Dreamliner, ili kuongeza ufanisi kwenye usafiri wa anga nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button