Serikali kuendelea kushirikiana na makanisa

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema serikali inatambua mchango wa makanisa nchini katika kuimarisha ustawi wa jamii.

Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa, George Chiteto.

“Serikali inatambua kazi inayofanywa na makanisa katika sekta mbalimbali, serikali tutaendelea kutoa ushirikiano kwenu,” alisema.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Maalumu, George Mkuchika alilipongeza Kanisa la Anglikana kwa kuendelea kufuata taratibu na katiba ya kanisa.

Kwa upande wake Askofu wa Dayosisi ya Mpwapwa, George Chiteto alisema alitaka makundi yaliyokuwapo kufutika baada ya uchaguzi kumalizika.

“Uchaguzi umekwisha hivyo makundi yaliyokuwepo yamefutwa rasmi, nitumie fursa hii kuomba ushirikiano.”

“Mimi ndiye Askofu nitakwenda kufanya kazi kwa ushirikiano, umoja ili kazi ya Mungu iende na kutimiza kusudi lake kila mmoja afanye wajibu wake bila kusukumwa na ninaahidi kuwa nitahudumia watu wote bila kubagua.”

 

Habari Zifananazo

Back to top button