Serikali imesema inaendelea kuimarisha masoko ya mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde amebainisha hayo leo bungeni jijini Dodoma alipojibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Stella Fiyao lililotaka ufafanuzi mkakati wa serikali wa kutafuta masoko ya mazao ya kilimo.
Amesema kuwa uimarishaji huo wa masoko utajikita katika kujenga masoko ya kimkakati mipakani,ujenzi wa vituo vya masoko na uboreshaji wa maabara za TPHPA.
Aidha, Mavunde amebainisha kuwa serikali inaendelea na mazungumzo na nchi mbalimbali kwa ajili ya kufungua masoko ya mazao katika nchi hizo.
“Hadi sasa serikali imefungua soko la korosho nchini Marekani, soko la parachichi China, India na Afrika Kusini na tunaendelea kuhudumia masoko ya nafaka katika nchi mbalimbali barani Afrika,” amesema Mavunde.