Serikali kuiwezesha TaSUBa

PWANI: SERIKALI imeendelea kuiboresha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kutoa fedha za kuboresha miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia kutokana na ukweli kuwa TaSuBa ni kitovu cha mafunzo katika tasnia za Sanaa na Utamaduni nchini.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko alipomwakilisha, Rais Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Tamasha la 42 la Kimataifa la TaSuBa lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na TaSUBa mkoani Pwani Oktoba 28, 2023.

“Niwapongeze Wizara kwa kuitangaza nchi yetu kwa kupitia kazi mbalimbali za utamaduni, sanaa na michezo. Aidha nakupongeza Waziri na wafanyakazi wa Wizara yako kwa kazi kubwa mnayoifanya kila mwaka katika kuliandaa na kuliendesha Tamasha hili kwa kipindi cha miaka 42 sasa,” amesema Dk Biteko.

Ameongeza kuwa, tamasha hilo lina hadhi kitaifa na kimataifa kwani limehusisha ushiriki wa vikundi vingi vya sanaa vya hapa nchini na vya kutoka nje ya nchi zikiwemo Zambia, Kenya, Burundi, Uganda, Botswana, Afrika Kusini, Canada na nyinginezo.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuwa, tamasha hilo limekua na mafanikio makubwa kwa Bagamoyo na mkoa wa Pwani. Amesema wadau wamejitokeza kwa wingi na kulifanya liwe tamasha bora nchini.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema kuwa, tamasha hilo ni fursa ya kutangaza utalii uliopo nchini kwa kuwakutanisha wadau kutoka ndani na nje ya nchi. Amesisitiza kuwa mwaka 2024 tamasha litakuwa kubwa kwa kuwaleta wadau wengi zaidi nchini.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Www.BizWork1.Com
1 month ago

Making additional money each month by performing a simple online task. Just by dedicating two hours a day to my home-based profession, I was able to earn and get $18,539 last month. Simple enough that even a youngster may learn how to do it and begin earning money online.
.
.
Detail Here———————————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x