SERIKALI imekusudia kujenga mabwawa makubwa mapya 14 nchi nzima kwajili ya Kufanya kilimo cha umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua.
Katika kufanikisha mpango huo, Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony mavunde amewataka wajasiliamali wakina mama wa Dodoma mjini kujiunga na program ya kilimo ya ‘BBT’ pamoja na kushiriki kwenye shughuli za kilimo.
Mavunde ameyasema hayo wakati wa Kongamano la Wajisiamali wakina mama wa Mkoa wa Dodoma, likilofanyika Dodoma leo Machi 28, 2023.
Amesema kwa kutambua fursa na mipango ya serikali kwenye sekta ya kilimo kwa wanawake wanapaswa kushiriki kwenye shughuli za kilimo.
Comments are closed.