Gofu Dodoma? Ondoa shaka uwanja unajengwa

SERIKALI imepanga kujenga uwanja mpya wa kimatafa wa gofu katika eneo la Chamwino jijini Dodoma.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro ametoa taarifa hiyo leo Novemba 23, 2023 jijini Arusha wakati akifungua Mashindano ya Kimataifa ya Gofu ya NCBA.

Amesema tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo juu ya ujenzi wa uwanja huo ambao utachangia kuibua vipaji na kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.

Mashindano hayo yatafanyika kwa siku nne ambapo wachezaji wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali wanashiriki ikwemo, Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Ethiopia na Zambia ambapo zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu kutoka kwa waandaaji zinashindaniwa.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *