Serikali kulinda vyanzo vya maji

WIZARA ya Maji imejipanga kuhakikisha vyanzo vyote vya maji vinalindwa ili kuwezesha upatinajani wa huduma ya maji.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ilipofanya ziara  mjini Morogoro .

Mhandisi Mahundi aliambatana na kamati hiyo kukagua bwawa la Mindu linalotarajiwa kuboreshwa zaidi ili kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji yenye kutosheleza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Alisema bwawa hilo ni chanzo kikubwa cha maji kinachotegemewa na wakazi wa manispaa hiyo kwa asilimia 75.

Mhandisi Mahundi alisema uhai wa binadamu kwa kiasi kikubwa unategemea maji na ili maji yapatikane kwa uhakika lazima sekta zote zishirikiane katika suala la utunzaji wa vyanzo vya maji vilivyopo maeneo mbalimbali nchi.

Naibu Waziri alizitaja miongoni mwa sekta hizo ni ya ardhi, misitu, mazingira, kilimo na nyingine mtambuka ambazo kwa njia moja au nyingine zinahusika moja kwa moja na huduma ya maji.

Naye Kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo ,Felix Kavejuru aliitaka serikali ya Mkoa wa Morogoro kusimamia vyema fedha za miradi mbalimbali ya maji Ili ilingane na thamani halisi ya fedha zinazotolewa kwa miradi hiyo.

Akitoa taarifa ya mradi wa ukarabati wa bwawa hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), Mhandisi Tamimu Katakweba alisema kukamilika kwa ujenzi wa kunyanyua tuta katika bwawa la Mindu ni suluhisho la utosherevu wa maji katika manispaa hiyo .

Mhandisi Katakweba alisema ujenzi huo unatokana na kutekelezwa kwa mradi wa matokeo ya kati chini ya ufadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) wa Sh bilioni 185.

Mhandisi Katakweba alisema mradi huo ni wa Kuboresha bwawa la Mindu kwa kunyanyua tuta mita 2.5 na miundombinu ukiwemo ujemlnzi wa mtambo wa kutibu maji eneo la Mafiga.

Mbali na mradi huo mkubwa alisema serikali inatarajia kutumia kiasi cha sh bilioni 225 za kuboresha huduma ya maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Morogoro .

Mhandisi Katakweba alisema kuwa miradi hiyo yote itakapo kamilika inawezesha upatikanaji wa huduma ya maji kuongezeka kutoka asilimia 62.5 za sasa na kufikia asilimia 96.

” Tunamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha itolewe kwa ajili ya ukarabati wa bwawa la Mindu ambalo ndiyo tegemeo la Manispaa ya Morogoro “alisema Mhandisi Katakweba

Awali Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmassy alisema kwa upande wao wameanza kuondoa makazi ya watu kandokando ya bwawa hilo pamoja na upandaji wa miti rafiki wa mazingira na vyanzo vya maji Ili kurejesha uoto wa asili.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work AT Home
Work AT Home
1 month ago

I am making $100 an hour working from home. I never imagined that it was honest to goodness yet my closest companion is earning $16,000 a month by working on a laptop, that was really dumbfounding for me, she prescribed for me to attempt it simply. Everybody must try this for this job now by just using

this site link… http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Work AT Home
AmberRuiz
AmberRuiz
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by AmberRuiz
CandidaDorean
CandidaDorean
1 month ago

★ I’m currently generating over $35,100 a month thanks to one small internet job, therefore I really like your work! I am aware that with a beginning capital of $28,800, you are presently making a sizeable quantity of money online.( s02w)
Just open the link══════►►► http://Www.SmartCareer1.com

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x