Serikali kumaliza foleni kwenye mizani

BUNDA, Mara: Serikali inatarajia kutenga Sh bilioni 81 kwa ajili ya ujenzi wa mizani ya kupima magari yakiwa kwenye mwendo (weigh in motion) kote nchini ili kuondoa msongamano na kupunguza muda wa kupima magari.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema hayo wilayani Bunda mkoani Mara wakati akikagua mradi wa ujenzi wa mzani wa kupima magari wa Rubana.
“Tathmini tuliyoifanya ya kubadilisha mizani yote nchini kwenye miaka mitatu ijayo ya bajeti kuanzia mwaka 2024/25 tuweke bajeti kwa awamu, hiyo bajeti ya Sh bilioni 81 tuigawe kwa tatu ili kila mwaka tuwe na kiasi cha fedha kwa ajili ya utekelezaji,” alisema Waziri Bashungwa akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi.
Waziri amesema lengo la serikali ni kuhakikisha mizani yote nchini ambayo haina iwezo wa kupima Magari yakiwa kwenye mwendo inakuwa ni ya kisasa, kwamba tathimini ya gharama ya utekelezaji imeshafanyika.
“Hivi sasa tunajua kwamba mizani yote nchini ili iwe na weigh in motion ambayo gari haliitaji kupanga foleni ili kujua limebeba uzito kiasi gani tathimini tuliyoifanya tunahitaji kuweka kwenye mizani yote nchini kwa gharama ya Sh bilioni 81,” alisema Bashungwa.

Habari Zifananazo

Back to top button