Serikali kuondoa shida ya maji machafu Mtwara

SERIKALI imesema inashughulikia changamoto ya maji kutoka machafu kwa baadhi ya mabomba yaliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani ili wananchi waendelee kutumia maji masafi kama ilivyo kawaida.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 7, 2023 na Naibu Waziri wa Maji, Maryspisca Mahundi bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Malapo aliyetaka kujua lini Serikali itakamilisha ujenzi wa chujio la maji katika manispaa hiyo.

Mahundi amesema Serikali imekamilisha ujenzi wa chujio hilo tangu mwezi Aprili, 2022. Hata hivyo Mbunge huyo alihoji ni kwanini maji yanatoka machafu licha ya taarifa za kukamilika kwa chujio hilo.?

Akijibu swali hilo la nyongeza, Maryprisca Mahundi amesema: “Swala la maji kutoka machafu baada ya ukamilishaji wa chujio ni suala la kiufundi, ni sehemu chache ambazo mabomba ni chakavu wakati fulani yanaleta udongo kwa ndani, lakini tayari watendaji wetu wanalifanyia kazi.”

Habari Zifananazo

Back to top button