Serikali kuongeza safari za treni Dar

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kutokana na changamoto ya usafiri inayowakabili wakazi wa Gongo la mboto na maeneo jirani, serikali ina mkakati wa kuongeza safari za treni ili kukabiliana na adha hiyo.

Akizungumza leo Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Chalamila amesema: “Jana nilitembelea Kamata nimeona jinsi watu wengi wanavyogombania treni kufika maeneo wanayoishi. Serikali ina mkakati wa kuboresha usafiri huu ikiwemo kuongeza safari za treni na mabehewa kuwezesha wananchi wa maeneo haya kunufaika.”

Pia amesema ukamilishaji wa barabara za mwendokasi awamu ya tatu kutoka Gerezani hadi Gongo la Mboto umegharimu Sh bilioni 231.5 utasaidia kupunguza adha ya usafiri kwa kiasi kikubwa

Amesema kuwa awamu ya tatu ya ujenzi wa mwendokasi utasaidia wakazi wa Gongo la Mboto, Chanika na Chamazi.

Pia ameeleza kuwa mipango ya baadaye ni kujenga barabara za mwendokasi kutoka Maktaba hadi Ohio, Ohio-Morocco na Morocco -Tegeta sawa na Kilometa 30.1 pia watajenga barabara ya Sam Nujoma na upanuzi wa barabara ya Kimara.

“Serikali imetumia fedha kutoka Benki ya Dunia, IMF na nyingine zinatokana na vyanzo vya ndani vya mapato. Barabara ya Gerezani- Mbagala yenye urefu wa Kilometa 20.3, imegharimu Sh bilioni 217,” ameeleza.

Aliongeza kuwa kutokana na adha ya usafiri kwa wakazi wanaoelekea Gongo la mboto na maeneo ya jirani, serikali ina mkakati wa kuongeza usafiri wa treni ili kusaidia wananchi wa maeneo hayo.

Habari Zifananazo

8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button