SERIKALI imesema itaendelea na mpango wa kuongeza udahili kwa wanafunzi wa kike kupitia mpango wa kuongeza fursa za ziada kwa wanawake katika programu za sayansi, uhandisi, hisabati na tiba.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo amesema hayo katika hotuba yake baada ya kushuhudia utiaji saini wa hati ya mikataba miwili ushirikiano baina ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) cha Butiama halfa iliyofanyika Kampasi kuu ya Edward Moringe Morogoro.
“Katika ngazi ya wizara tumetoa Dk Samia Scholarship kuweza kuwahamasisha wanafunzi wakike kujiunga katika kozi za sayansi , teknolojia , hisabati na zile za tiba.
” alisema Prof Profesa Nombo
Prof Nombo amesema kutokana uhamasishaji huo kwa wanafunzi wa kike kujiunga katika programu za sayansi, uhandisi, hisabati na tiba, katika awamu ya kwanza takribani wanafunzi wa kike 700 wamenufaika na ufadhili huo.
Amesema kwa mwaka huu wa masomo, wizara imetenga fedha kwa ajili ya kutoa ufadhili kwa wanafunzi wakike wengine 700 .
“ Tumetenga tena bajeti ya fedha kwa walengwa ambao wataingia kwenye fani hizo za programu za sayansi, uhandisi, hisabati na tiba … ni fursa kwa wanafunzi wa kike kushiriki kwemye janya hizi “ amesema Profesa Nombo.