WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imeona umuhimu na faida kubwa ya kubangua korosho nchini na sasa imedhamiria kurudisha viwanda vya zao hilo ili manufaa yabaki Tanzania.
Majaliwa amesema hayo leo mara baada ya kutembelea kwanda cha kubagua korosho kilichopo Wilaya ya Tandahimba Mtwara.
“Sasa tumeshtuka, tunataka turudishe viwanda ili manufaa yabaki Tanzania, anayetaka Korosho aje anunue mbegu ya Korosho hapa tukiwa tumefunga kwenye nusu kilo, kilo mbili na kilo tatu.” amesema.
Majaliwa amesema Raisi Samia Suluhu Hassan amesisistiza na kutaka kuona Tanzania inauza korosho zilizobaguliwa nchini kuliko kuuza korosho ghafi.
“Kuuza korosho ghafi nje ya nchi tunaondoa utajiri woote tunapeleke India,” amesema.
Majaliwa amefika Mtwara jana na kuendeleza ziara yake ya kikazi katika Wilaya za Tandahimba, Newala, Masasi na Nanyumbu.