Serikali kushawishi uwekezaji nishati

DODOMA: SERIKALI imesema itahakikisha inaweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya nishati ili kuchochea maendeleo ya uchumi.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametoa hakikisho hilo leo Oktoba 05, 2023 katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa ushirikiano kwenye sekta hiyo kati ya Tanzania na Uswidi ‘Sweden’ kwa miaka 60.

Advertisement

Pamoja na mambo mengine amesema kuwa Sweden imekuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya nishati hususani ya umeme.


“Sweden ni moja ya nchi muhimu inayochangia kwa kiasi kikubwa kwenye miradi ya nishati hususani umeme,” amesema Biteko.

Amesema, Sweden imechangia Sh bilioni 142 kwenye miradi ya ujazilizi katika vitongoji 1328 na Sh bilioni 52 kwa vijiji 151.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *