Serikali kushughulika na waharibifu wa mazingira

SERIKALI imesema itahakikisha inawachukulia hatua waharibifu wa mazingira wanaofanya shughuli za uchomaji wa misitu, ukataji miti, uharibifu wa maeneo ya hifadhi na vyanzo vya maji.

Hayo yameelezwa leo Februari 8, 2023 na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Asha Juma aliyetaka kujua dhamira ya Serikali katika kuwapa watu elimu ya uokozi na uhifadhi badala ya kutegemea JWTZ na Jeshi la Uokozi pekee.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Naibu Waziri Khamis Khamis amesema Serikali imekusudia kuwaelimisha wananchi juu ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi baada ya kufanya shughuli za kibinadamu.

“Mbali na kuwaelimisha kwa vile sheria zipo, tatu ni kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote wanaochafua ili lengo na madhumuni tusiwape mzigo JWTZ na zimamoto.” amesema Khamis Khamis.

Habari Zifananazo

Back to top button