WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Doroth Gwajima amesema serikali itatunga sheria na sera ambazo zitalenga kuwasaidia wafanyabishara wa chakula maarufu kama mama ntilie.
Dk Gwajima alisema katika mapitio hayo watawashirikisha wadau wote wakiwemo mama ntilie.
Gwajima alisema watafanya kikao kwa kushirikiana na wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuwa kazi hiyo ni mtambuka.
“Tutatengeneza ripoti kujua ni mama ntilie wangapi wanapata mikopo inayotolewa na serikali tutafuatilia kwani serikali imetoa bilioni 26 kwa wanawake; tutafuatilia kujua walipata wangapi na ambao hawajapata kwanini,” alisema Dk Gwajima.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Jikoni Business, Nice Mamuya alisema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo Wameweza kuhamasisha mama ntilie kwa kuanzisha fursa,kufanya hamasa kwenye masoko,kuelimisha na kusajili,kutafuta wafadhili ili wanafanye biashara.
“Changamoto zilizopo ni utambuzi katika maeneo mbalimbali na kuwa watu baki inatokana kutikuwepo kwa Taasisi zinazowatetea”alisema Mamuya na akaishukuru serikali kwa kuahidi kushughukia changamoto zinazowakabili.