Serikali kuwaangalia wanaojitolea huduma za afya

SERIKALI itaangalia uwezekano wa kuanzisha ‘Data Base’ kwa ajili kuwatambua wahudumu wa afya ambao wanafanya kazi kwa kujitolea ili baadaye kupewa kipaumbele pindi nafasi za ajila zitakapotoka.

Hayo yamesemwa leo Aprili 6, 2023 na Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Felister Njau aliyehoji serikali haioni umuhimu wa kutengeneza “Data base” ili kutambua wahudumu wote wanaojitolea ili wakati ajira waweze kupewa kipaumbele.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Godwin Mollel amesema wizara imepokea ushauri huo na watashirikiana na Wizara ya Utumishi kwa ajili ya ufumbuzi zaidi.

Aidha, Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson, amesitizia katika suala hilo kwa kusema Waziri wa Afya na Wizara ya TAMISEMI wanahaja ya kukaa pamoja na Ofisi ya Rais, Utumishi na utawala Bora kwa sababu watumishi wa afya wanaojitolea na walimu wanaojitolea shule za msingi na sekondari hivyo haipendezi kuona wanaojitolea wanakosa sifa za kuwajiriwa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x