Serikali kuwasilisha bajeti yake Alhamisi

SERIKALI inatarajiwa kuwasilisha mapendekezo ya bajeti yake mwaka 2024/2025 wiki hii.

Bajeti hiyo itakayosomwa Alhamisi na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, itakuwa ni ya tatu tangu Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani.

Usomwaji wa mapendekezo ya bajeti hiyo utatanguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya RaisMipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo atakayesoma taarifa ya hali ya uchumi.

Bajeti itakuwa na kitabu cha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya kawaida kwa wizara, idara zinazojitegemea na wakala za serikali.

Pia makadirio ya matumizi ya kawaida kwa sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa na makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa wizara, idara zinazojitegemea, wakala wa serikali, sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa.

Wakati wa kujadili makadirio ya mapato na matumizi, wabunge walishauri kuongezwa fedha katika sekta ya maji. Pia walishauri Sh bilioni 14 kati ya Sh bilioni 19 zilizoongezwa kwenye Wizara ya Maliasi na Utalii zipelekwe kwenyemaendeleo.

Hoja nyingine zinazotarajiwa kuzungumziwa ni pamoja na uhaba wa watumishi, madeni ya wazabuni na wakandarasi, urekebishaji wa barabara zilizoharibiwa na mvua.

Machi mwaka huu, serikali iliwasilisha kwenye Kamati ya Bunge zima mapendekezo ya bajeti kuu kuwa Sh trilioni 49.345.7 kwa mwaka 2024/2025, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/2024 ya Sh trilion 44.388.1.

Kati ya mapato hayo, mapato yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania yanakadiriwa kuwa Sh trilioni 29.858.4 huku mapato yasiyo ya kodi yanayokusanywa na wizara, taasisi na idara zinazojitegemea ni Sh trilioni 3. 408.1.

Mapato ya mamlaka za serikali za mitaa ni Sh trilioni 344.1.19. Makadirio hayo yamezingatia vigezo mbalimbali ikiwamo mwenendo halisi wa ukusanyaji wa mapato , viashiria vya uchumi jumla na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Aidha, sehemu kubwa ya bajeti (asilimia 70.1) itagharimiwa na mapato ya ndani ambayo yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 10.

Habari Zifananazo

Back to top button