Serikali na mipango ya kukipaisha Kiswahili

DAR ES SALAAM: KATIKA mwaka ujao wa fedha mkakati wa serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ni kutoa ajira kwa Watanzania kote duniani kupitia lugha ya Kiswahili lengo ni kuendelea kuipaisha lugha hiyo na kuipa thamani zaidi.

Kauli hiyo imetolewa Oktoba 16,2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro wakati alipofanya ziara katika ofisi za Baraza la Kiswahili BAKITA jijini Dar es salaam ambapo amesema BAKITA itazunguka dunia nzima kutoa mafunzo mafupi kwa wanadiaspora ili waweze kuwafundisha wageni.

Amesema Kiswahili kwa sasa kinashika nafasi ya 10 Duniani na mipango endelevu waliyonayo ni kukifanya Kiswahili kiingie katika lugha tano maalumu Duniani.

Advertisement

Aidha ameongeza kuwa mkakati mwingine walionao ni kushirikiana na vyuo vyote duniani na Taasisi nyingine kuhakikisha kuwa kuna vituo vingi vya kufundisha lugha ya Kiswahili kila nchi.

Awali Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Consolatha Mushi ameeleza kuwa, katika mkakati wa miaka kumi wa kukipa thamani Kiswahili wa 2022 – 2032, tayari wamefungua vituo 32 ambavyo vituo 10 vipo katika Balozi za Tanzania na tayari limepokea maombi ya kuanzisha vituo vya kujifunza lugha hiyo kwa nchi za Ufaransa na Uturuki.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *