Serikali yaahidi jambo Shule ya Miwa

KILOSA, Morogoro: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameahidi kupeleka walimu katika Shule ya Sekondari Miwa iliyopo wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro ili kutatua changamoto ya walimu shuleni hapo.

Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa (mbele kulia) akiwa ziarani na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima

Waziri Mchengerwa amesema hayo wakati wa ziara yake wilayani humo na kutembelea Shule ya Sekondari Miwa iliyojengwa kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu Msingi na Sekondari (SEQUIP).

Soma pia: https://habarileo.co.tz/ajira-1500-za-walimu-posho-nono/

Ahadi ya Mchengerwa imetokana na ombi lililotolewa na dada mkuu wa shule hiyo, ambaye pamoja na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule ameiomba Serikali iwapatie walimu kutokana na changamoto ya uhaba wa walimu iliyopo shuleni hapo.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7OdLgZuzsp/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Akijibu hoja ya dada mkuu huyo, Mchengerwa amesema mara mchakato wa ajira utakapokamilika atahakikisha kuwa shule hiyo inapatiwa walimu wa kutosha kufundisha wanafunzi hao wenye kiu ya elimu.

Shule hiyo mpya imetatua changamoto kwa wanafunzi ya kutembea umbali wa kilomita 26 kila siku kwenda na kurudi shuleni katika Kata ya Luhembe.

Habari Zifananazo

Back to top button