Serikali yadhamiria uzalishaji korosho

SERIKALI imedhamiria kuongeza uzalishaji wa zao la korosho ghafi hadi kufikia tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/26 na kuongeza hadi kufikia tani milioni moja ifikapo mwaka 2029/30.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde wakati akifungua mkutano mkuu wa wadau wa korosho nchini unaofanyika mkoani Tanga amesema kuwa hiyo ni kutokana na ukweli kwamba zao hilo ndio linaloongoza kwa uzalishaji ukilinganisha na mazao mengine.

Amesema kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2022/23 zao hilo limeweza kuliingizia taifa fedha za kigeni Dola milioni 226.

Advertisement

9 kutokana na mauzo yake nje ya nchi ikifuatiwa na mazao mengine.

Amesema kuwa kutokana na mapato hayo inaonyesha kwanza zao hilo linamchango mkubwa wa uchumi wa taifa hili hivyo ni vema sasa serikali ikajipanga katika kuweka mipango bora ya kuongeza uzalishaji ili kupata mapato zao lakini na mkulima kuweza kunufaika na kilimo hicho.

“Sisi serikali ni lazima tusimame kidete na wadau wa zao hilo kuhakikisha tunashirikina katika kutatua changamoto za kimsingi zinazolikabili zao hilo ili uzalishaji uweze kuongezeka na kuyapima mafanikio hayo kupitia uchumi wa mkulima mmoja mmoja pamoja na uchumi wa Taifa hili kwa ujumla.

5 comments

Comments are closed.