Serikali yaelekeza pambano la Mwakinyo lifuatiliwe

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa, amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kufuatilia tukio la pambano la ngumi kati ya bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo dhidi ya bondia wa Uingereza Liam Smith lililofanyika nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kupitia kitengo cha Mawasiliano serikalini cha  wizara hiyo, imesema hatua hiyo ina lengo la kubaini hali ya sintofahamu iliyojitokeza katika pambano hilo.

Taarifa imesema serikali haipo tayari kuona mazingira yoyote ya sintofahamu kwa wachezaji wa kitanzania wanaposhiriki mashindano hasa ya kimataifa.

Habari Zifananazo

Back to top button