Serikali yafafanua huduma kwa watoto njiti

SERIKALI imesema utoaji wa huduma za afya kwa watoto chini ya miaka mitano wakiwepo watoto njiti kwa vituo vya serikali na vile vya binafsi vilivyo na ubia na serikali ni bure na ni takwa la Sera ya Afya.

Hayo yamesemwa leo Februari 7, 2023 na Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel akijibu swali ma Mbunge wa viti maalum Agness Hokororo aliyetaka kujua iwapo serikali ipo tayari kurejesha gharama walizolipa wanawake waliojifungua Watoto njiti.

“Kwa nini huduma za afya kwa watoto njiti zinatozwa fedha ihali sera ya afya ni huduma bure kwa watoto chini ya miaka mitano…..Je Serikali iko tayari kurejesha fedha kwa wanawake wajawazito. Ninayo madai ya anayedaiwa Sh milioni 1.8 katika Hospitali ya Muhimbili.” Alihoji

Akijibu Mollel amesema atalifuatilia bila kuahidi kurejesha fedha hizo na kwamba kama serikali wataangalia namna watakavyolifanya na iwapo watabaini aliyefanya hivyo basi atapewa maelekezo.

Mollel amesisitiza kuwa Mswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote utamaliza utata huo kwa wananchi wanaotibiwa katika vituo binafsi vya huduma za Afya.

Habari Zifananazo

Back to top button