Serikali yafafanua nusu kaputi kuhusishwa na vifo
…hata hivyo vifo vya namna hii hutokea mara chache sana na ndio maana wakati wote tunawashauri akina mama wajawazito kuhudhuria kliniki ili kutoa kutoa muda wa kutosha kufuatiliwa na pale itakapohitajika kufanyiwa upasuaji usiwe wa dharura
SERIKALI imeeleza kuwa kuna sababu tatu zinazochangia vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua kwa upasuaji.
Akizungumza wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu bungeni, Dodoma leo asubuhi, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ametaja miongoni mwa sababu hizo ni sababu za nasaba (DNA).
Nyingine ni zile zinazolhusishwa na ganzi, japo si sababu ya moja kwa moja pamoja na Sababu zenye mahusiano ya moja kwa moja na ganzi.
Naibu Waziri ametoa maelezo hayo wakati akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Dk Christina Mnzava aliyetaka kufahamu ikiwa kuna utafiti wowote ambao umefanyika ili kubaini dawa za ganzi/nusu kaputi zinazosababisha vifo kwa wanaojifungua kwa upasuaji.
“…hata hivyo vifo vya namna hii hutokea mara chache sana na ndio maana wakati wote tunawashauri akina mama wajawazito kuhudhuria kliniki ili kutoa kutoa muda wa kutosha kufuatiliwa na pale itakapohitajika kufanyiwa upasuaji usiwe wa dharura,” ameeleza.
Hata hivyo, Naibu Waziri ametoa wito kwa jamii kuhakikisha kuwa inahamaisha kutoa lishe bora kwa wajawazito.