Serikali yafafanua Sh bilioni 7.5 ukarabati MV Magogoni
SERIKALI imesema Sh bilioni 7.5 za ukarabati wa Kivuko cha MV. Magogoni zitahusisha ununuzi wa injini 5 mpya Injini 4 zitafungwa kwenye kivuko na Injini 1 ya akiba.
Taarifa ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imefafanua kuwa ukarabati huo pia utahusisha kufungwa ‘marine steel plates mpya, Gear box mpya, vifaa vya umeme na kielektronic vipya na kivuko kitadumu kwa miaka 14 au zaidi.
Taarifa ya Wizara imeeleza kuwa zabuni ya ukarabati ilipewa kampuni ya African Marine and General Engineering Company Limited ya Mombasa nchini Kenya, ambayo iliomba kufanya kazi kwa gharama ya Sh bilioni 7.
5 na kuachana na Kampuni ya Songoro Marine Transport LTD ya Mwanza Tanzania ambayo iliomba kufanya kazi hiyo kwa gharama ya zaidi ya bilioni 10.
Baada ya kushindanishwa Serikali ilimpa kazi hiyo ya ukarabati mkubwa mzabuni namba moja ambaye ni African Marine and General Engineering Company Limited. Mkataba wa kazi hiyo ni wa siku 180 sawa na miezi 6.
Kivuko MV Magogoni kinachofanyiwa ukarabati mkubwa kina uwezo wa kubeba tani 500, (abiria 2,000 na magari 60).