MANYARA; JUMLA majeruhi 117 walipokelewa katika Kituo cha Afya Gendabi, Hospitali ya Tumaini iliyopo Wilaya ya Hanang na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.
Msemaji wa Serikali Mobhare Matinyi akizungumza leo Desemba 5, 2023, amesema kati ya majeruhi hao 18 hawakuwa na hali nzuri na walihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa matibabu zaidi, ambapo mmoja kati yao alifariki dunia jana saa nne usiku.
Akitoa mchanganuo huo Matinyi amesema majeruhi 117 hadi kufikia asubuhi ya leo Desemba 5 watu wazima 61, Wanaume 30; wanawake 31, upande wa watoto waliojeruhiwa hadi sasa ni 56 kati yao wa kiume 27 na wa kike 29.
Amesema jumla ya miili 65 ilipokelewa na kuhifadhiwa katika Kituo cha Afya Simbay, Kituo cha Afya Magugu, Hospitali ya Dareda, Hospitali ya Mji wa
Babati, Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini), na Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Manyara.
Amesema mchanganuo wa vifo hivyo marehemu 65 waliopokelewa hadi kufikia
asubuhi ya leo, ambapo watu wazima ni 41 kati yao wanaume 15 na wanawake 26, huku watoto wakiwa ni 24 wa kiume 10 na wa kike 14.
Wakati huo huo, Matinyi amesema kuwa kambi za waathirika hadi sasa kuna jumla ya waathirika 190, ambapo katika shule ya shule ya Sekondari Katesh ni 118 wanaume Wanaume 46 na wanawake 72.
Shule ya Msingi Gendabi ni 66 wanaume 40 na Wanawake; 14, watoto wa kiume wanne na watoto wa kike ni nane wakati shule ya Msingi Ganana ni sita wanaume wawili na wanawake wanne.
“Hawa wanatarajiwa kuhamishiwa kwenye kituo cha Shule ya Sekondari
Katesh kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa huduma,”amesema Matinyi.
Comments are closed.