Serikali yafanya tathmini ya elimu nchini

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe ameungana na timu ya Ufuatiliaji wa Kisekta, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na wadau wa Elimu ili kufanya tathmini ya masuala ya elimu nchini.

Timu hiyo imekutana jijini Arusha jana kwa lengo la kufanya tathmini ya kina kuhusu matumizi ya TEHAMA katika shule za msingi na sekondari.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari leo Septemba 20, 2022 Prof Shemdoe amesema tathmini hiyo itawahusisha wanafunzi, walimu, wazazi na kamati pamoja na Bodi za shule kwenye shule zinazo tumia TEHAMA na zile ambazo hazitumii ili kuona kama kuna manufaa ya matumizi ya TEHAMA kwenye kuboresha Elimu na ujifunzaji.

“Kwa shule na wadau watakao tembelewa wahakikishe wanatoa taarifa sahihi ili kuiwezesha Serikali kuona namna bora ya kuboresha namna ya ujifunzaji katika shule za Umma.”Amesema

Aidha, Shemdoe amewataka pia wajumbe wa Menejimeti ya Halmashauri ya Jiji la Arusha na Mamlaka nyingine za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanajibu hoja za ukaguzi na kwamba suala la ukusanyaji wa mapato na kujibu hoja za ukaguzi ziwe agenda za kudumu katika vikao vyao.

Amesema watumishi wanapohamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine si adhabu bali wanahamishwa kwenda kuongeza nguvu ya utendaji kwenye kituo kingine ili kuwatumikia wananchi

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x