Serikali yaja kivingine malalamiko ya walipa kodi

DAR ES SALAAM: SERIKALI imeanzisha taasisi ya usuluhishi wa malalamiko na taarifa za Kodi (TOST) ambayo itatoa huduma zake kwa umma katika masuala yote yanayohusu malalamiko ya waliopata kodi kuhusiana na taratibu za usimamizi wa sheria za kodi.

Aidha taasisi ambayo iko chini ya Wizara ya Fedha itashughulikia pia utoaji wa huduma na maamuzi mbalimbali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akizungumzia taasisi hiyo leo Dar es Salaam, Msuluhishi wa malalamiko na taarifa za Kodi, Robert Manyama amesema taasisi hiyo imeanzishwa kama jukwaa huru la kutoa usuluhishi wa malalamiko na taarifa za kodi kwa kuzingatia haki na usawa Kwa mlalamikaji na mlalamikiwa.

Advertisement

” usuluhishi wa malalamiko ya kodi Kwa wakati utapunguza kwa kiasi kikubwa pingamizi za kodi na migogoro ambayo isiyo na ulazima wa kupelekwa mahakamani,’ amesema Manyama na kuongeza kuwa sheria iliyoundwa taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2019 Kwa marekebisho yaliyofanywa katika sheria ya usimamizi wa kodi 2015.

Amesema dhamira ya taasisi hiyo ni kushughulikia malalamiko ya kodi kwa usawa na kwa ufanisi,kutatua malalamiko dhidi ya usimamizi wa sheria za kodi Kwa njia ya majadiliano na upatanishi au kwa njia ya nyingine zisizo rasmi.

Meneja wa TOST, Naomi Mwaipola amesema huduma za Taasisi hiyo zinamfikia yoyote atakayetoa malalamiko na kwamba Kila mmoja anaruhusiwa kupeleka malalamiko anayokumbana nayo.

1 comments

Comments are closed.