Serikali yakabidhi kijiji cha Msomera, Kilindi na Handeni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imekabidhi rasmi kijiji cha Msomera kwa Wilaya za Handeni na Kilindi mkoani Tanga ukiwa ni mpango wa kuendeleza kijiji hicho ambacho wakazi wake wengi ni wananchi waliohamia kwa hiari kutoka katika eneo la Uhifadhi Ngorongoro mkoani Arusha.

Waziri Majaliwa amesema hayo wakati akiongea na mawaziri wa kisekta, wakuu wa mikoa ya Tanga na Arusha, viongozi wa kimila na wawakilishi wa wananchi Kijiji cha Msomela wilayani Handeni.

“Leo nimekuja kuwakabidhi rasmi mradi huu wa Kijiji Cha Msomera muweze kuuingiza kwenye mipango yenu ya maendeleo kama ambavyo serikali kuu imeweza kufanya”amesema Waziri Mkuu.

Advertisement

Aliyekuwa Naibu Waziri wa mifugo ambaye amehamia kutoka Ngorongoro Kaika Ole Telele amesema kuwa uamuzi wa serikali kuwahamisha kuja kwenye Kijiji hicho ni hatua ambayo itaacha alama kubwa kwa vizazi na vizazi.