Serikali yakabidhiwa vituo 5 kukabiliana na ukatili

VITUO vitano vipya vya kusaidia uwezeshaji wa wanawake kukabiliana na ukatili wa kijinsia vimekabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania katika mikoa ya Singida na Shinyanga lengo likiwa ni kusaidia kupambana na matukio hayo haramu katika jamii.

Vituo hivyo vimetolewa kwa msaada na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kwa kushirikia na na UN Women kwa ufadhili wa serikali Korea kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea (KOICA) chini ya Mpango wa Pamoja.

Akizungumza katika makabidhiano hayo MKurugenzi wa KOICA nchini Tanzania, Shin Manshik, amesema vituo hivyo vitawezesha kukuza mtazamo unaozingatia waathirika wa unyanyasaji kufikia huduma za afya, usaidizi wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia.

Amesema Vituo hivyo vitano nipamoja na vitatu vya One Stop Centre, Dawati moja la Jinsia na Watoto la Polisi, na Kituo kimoja cha Makusanyo, na mafunzo na programu zinazohusiana ambavyo tayari vimepanua kwa kiasi kikubwa uwezo wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Amesema Mpango huo wa Pamoja, uko katika mwaka wake wa mwisho ukianzia mwaka (2020-2023) ulifadhiliwa na KOICA kwa dola za Kimarekani milioni 4.9.

“Kupitia mpango huo zaidi ya watu elfu kumi wamefikiwa ili kuongeza ujuzi wa haki zao, kusaidia usawa wa kijinsia, na kupanua uwezo wa kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia na kuimarisha uwezeshaji wa wanawake kiuchumi katika mikoa ya Singida na Shinyanga,” amesema Manshik.

Amesema KOICA inatarajia kutoa huduma muhimu za kisheria, kijamii na kimatibabu kwa waathiriwa wa ukatili wa kijinsia kupitia Vituo vya Pamoja ambavyo vimejengwa.

Naibu Mwakilishi wa UNFPA, Melissa McNeil-Barrett, amesema uanzishwaji wa vituo hivyo vya One Stop Centre, na Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi vinawakilisha hatua kubwa katika kuimarisha taasisi za ndani ili kuzuia na kukabiliana na ukatili.

“Matarajio ya programu hii ni wazi katika kuongezeka kwa idadi ya kesi za ukatili wa kijinsia ambazo zitakuwa zinazoripotiwa na kuchukuliwa hatua.” Amesema.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake (UN-Women) Hodan Addou amesema uwezeshaji wa kiuchumi ni njia muhimu ya kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

Akipokea vituo hivyo, Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amesema mradi huo wa kufikia usawa wa kijinsia wa kwa kuwewezesha wanawake, wasichana balehe kwa kuwainua na kupinga vitendo vya ukatili utafikia wengi ambao walikuwa wahanga wakubwa

Habari Zifananazo

Back to top button