Serikali yaokoa fedha za matibabu kwa 72%

Watu 87 wawekewa puto Mloganzila

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema huduma za kibingwa zinazotolewa nchini ikiwemo upandikizaji uroto na na huduma za kibobezi za kupunguza uzito kwa kuweka puto, kumeokoa fedha za serikali kwa asilimia 72.

Akisoma Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2023/2024 na Hali ya Uchumi wa Taifa wa mwaka 202215, 2023 Nchemba amesema hali hiyo imetokana na serikali kuboresha huduma za kibingwa nchini kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wake.

Amesema, upatikanaji wa huduma hizo za kibingwa nchini umepunguza gharama za kupata huduma nje ya nchi kutoka shilingi milioni 250 hadi kufikia milioni 70 sawa na punguzo la asilimia 72 ya gharama zilizohitajika

Amesema jumla ya wagonjwa 87 wamepatiwa huduma ya kupunguza uzito kwa kuwekewa puto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili – Mloganzila.

Pia, amesema   jumla ya wagonjwa 25 wamepatiwa huduma za kibingwa za upandikizaji wa uroto katika hospitali za Muhimbili na Benjamin Mkapa.

Habari Zifananazo

Back to top button