Serikali yaombwa mkazo ndoa za utotoni

MTANDAO wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN),umeiomba serikali kuangalia uwezekano utakaozingatiwa na mapendekezo ya kamati ya wataalamu wa haki za watoto ya Afrika katika kuchukua hatua kutokomeza ndoa za utotoni.

Ombi hilo limetolewa mjini Morogoro kwenye kikao kilichojadili masuala mbalimbali ya Mtandao huo na kutolewa tamko kuhusu mchakato wa mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwakaa 1971.

Mratibu wa TECMN ,Euphomia Edward amesema ipo haja kwa serikali kuweka mkazo katika sheria za kuzuia ndoa za utotoni ili kupunguza idadi ya ndoa za utotoni hapa nchini.

Amesema mwezi wa sita mwaka huu (2022) , Wizara ya Katiba na Sheria ilitoa barua inayoelezea mchakato wa serikali wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu ndoa za utotoni.

Mratibu wa TECMN amesema ,mchakato huo umeleta sintofahamu miongoni mwa wadau zikiwemo AZAKI inazojihusisha na utetezi wa haki za mtoto , na taarifa za kina kuhusiana na mchakato huo hazijapatikana.

Kwa kuonesha ukubwa wa tatizo hilo amesema , kwa mujibu wa takwimu za Utafiti wa Demografia na Afya (TDHS) za mwaka 2015/2016 asilimia 36 ya wasichana hapa nchini wanolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 na hizo ni kwa ngazi ya Kitaifa

Utafiti wa Demografia na Afya pia uliainisha asilimia kwa kila kimikoa , na Shinyanya unaongoza kwa asilimia 59 ya wasichana wanaolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18 ukifuatiwa na Tabora asilimia 58 na mingine ni Mara na Dodoma.

“ Hili tatizo ni mkubwa na hawa wasichana wanaolewa wakiwa wadogo na wanakatishwa ndoto zao za kupata haki yao ya elimu , wanakuwa hawajakomaa nawanakuwepo kwenye hatari nyingine ya kufanyiwa ukatili” amesema Mratibu huyo

Mratibu wa TECMN amesema ukatili huo ni pamoja na vipigo kwenye ndoa ,ukatili wa kiuchumi kutokana na kukatishwa masomo kwani hawawezi kujitafutiaa kipato wala kulea familia.

“ Kwa kupata mimba za utotoni wanachangia kuiongezeka kwa vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi” amesema Mratibu wa TECMN

Habari Zifananazo

Back to top button