Serikali yaongeza majaji, mahakimu

SERIKALI imesema kuwa imeongeza idadi ya majaji wa mahakama ya rufaa kutoka 16 hadi 24 na wa mahakama kuu kutoka 78 hadi 98. Wakati huohuo idadi ya mahakimu iliongezeka kutoka mahakimu 245 hadi 293.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Serikali imeendelea kufanya maboresho mbalimbali ya kiutendaji pamoja na ujenzi wa miundombinu muhimu ya Mahakama kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji wa mahakama na kuimarisha mifumo ya utoaji haki.”amesema Majaliwa.

Advertisement