Serikali yapania uchumi wa kidijitali

SERIKALI inaendelea na jitihada za kukuza sekta ya mawasiliano ili kujenga uchumi shirikishi wa kidigitali.

Akizungumza katika uzinduzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini (Submarine Cable) wa 2 Afrika na Teknolojia ya Mawasiliano ya Kasi ya 5G ya Airtel Rais Samia Suluhu Hassan amesema uzinduzi wa teknolijia hiyo ya 5G utaongeza ukuaji wa sekta mbalimbali nchini.

Amesema, kutokana na umuhimu wa Tehama, teknolojia inaendelea kukua kwa kasi, serikali ya awamu ya sita imejidhatiti kuweka mazingira wezeshi kwa kutoa huduma za wawekezaji na kujenga miundombinu ya mawasiliano.

Amesema, hivi karibuni wameanza ujenzi wa minara 758 kwa ajili ya kupanua wigo wa mawasilino ambapo utawanufaisha watanzania milioni nane kote nchini mijini na vijijini.

“Nilikuwa naona 5G kama ndoto kufika nchini , nawapongeza Wizara sasa tumeshuhudia lidude lile likubwa linaitwa Robot linaleta 5G Tanzania.

“Wakati lile roboti linakuja kuleta 5G nilikuwa najiuliza ni mimi ndio nitalipokea au mwingine, maana lingeamua kutandika kibao na lilivyo kubwa sijui kama ningenyanyuka.

Amesema, takwimu za TCRA Machi 2023, kuna laini za simu Milioni 61, hii ni karibu ya watanzania wote wanatumia simu.

Amesema, kati ya line milioni 61, ni laini milioni 33 tu ndizo hutumia internet kupitia simu janja na vifaa vingine vya mawasiliano.

“Mkongo wa 2 Afrika utaweza kutuunganisha vizuri na dunia kwa sababu unaunganisha Mabara ya Asia, Ulaya na Afrika kwa urefu wa kilomita 45,000 na unakisiwa utatumiwa na watu zaidi ya bilioni 3 duniani, Tanzania ikiwemo na sisi ndio tutawapa huduma wenzetu nchi zisizo na bahari.”Amesema

Amesema, Mkongo huo mpya utachochea ushindani wa kibiashara na kufanya gharama za matumizi ya internet zipungue. Itafanya Tanzania iunganishwe na dunia muda wote.

“Tanzania kuwa kitovu cha mtandao kwa nchi zilizotuzunguka, itatoa fursa kwa watoa huduma za simu wachague mkongo upi watumie, jambo litakaloongeza ubora na kushuka kwa gharama maana kutakuwa na ushindani, mkongo wa zamani, na huu.

Aidha, Rais Samia amesema, kuwepo kwa huduma mbadala kutaifanya Tanzania kuunganishwa na dunia wakati wote.

Amesema, kwa kuzingatia mwelekeo wa nchi ushiriki uchumi wa kidigitali bado kuna mambo mengi kama nchi ya kufanya ikiwemo kuboreshwa zaidi kwa mifumo ndani ya serikali ili isomane.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button