Serikali yapendekeza bajeti ya sh trilioni 44.39

SERIKALI imependekeza mapato na matumizi ya Sh trilioni 44.39 kama bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema jumla ya mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Sh trilioni 31.

38, sawa na asilimia 70.7 ya bajeti yote.

Kati ya mapato hayo, mapato yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania yanakadiriwa kuwa Sh trilioni 26.73 na mapato yasiyo ya kodi (Wizara, Idara, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa) yanakadiriwa kuwa Sh trilioni 4.

66.

Habari Zifananazo

Back to top button