Serikali yapiga marufuku Kanga moko

atakayekiuka kuswekwa lupango

SERIKALI  ya Zanzibar kupitia Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni imepiga marufuku mtindo wa wanawake kulowesha kwenye maji kanga maarufu ‘Kanga Moko’ au nguo zao na kisha kucheza nazo mziki.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Omar Adam amesema kuna tabia imezuka watu kucheza mziki wakiwa wamelowesha nguo zao kwenye baadhi ya sherehe ama mikusanyiko.

Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt.Omar Adam amesema haya leo Julai 11, 2023 akihojiwa na ZBC kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Sanaa na Filamu na namna wanavyosimamia Mila, Desturi na Utamaduni wa Zanzibar.

Amesema, Zanzibar kwa siku moja huwa kuna shughuli 50 hadi 100 hivyo hilo hawawezi kuzuia.

“Hatujapiga marufuku kupiga muziki bali kupiga muziki kwa sauti iliyopitiliza na kucheza muziki kwa mitindo isiyofaa na inayopingana na desturi za Zanzibar hasa huu mtindo wa wakina Dada kucheza kwa kulowesha nguo maji, ni marufuku na Askari wana ruhusa ya kuwakamata.”Amesema

 

Habari Zifananazo

Back to top button