Serikali yapokea vichwa vitatu, mabehewa 27 treni ya umeme

SERIKALI imepokea vichwa vipya vitatu vya treni za umeme kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa mapya 27 ya abiria yaliyoundwa na kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) kutoka nchini Korea Kusini

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 30, 2023 na Shirika la Reli Tanzania (TRC) imeeleza kuwa licha ya serikali kufanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria shirika pia limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne kati ya 17 kutoka katika kampuni hizo.

“Mabehewa matatu (3) yaliyosalia yanatarajiwa kuwasili nchini Februari, 2024. Vichwa 13 vilivyobak i vinatarajiwa kuwasili kwa awamu kamaifuatavyo, vichwa sita (6) vitawasili mwezi Machi na vichwa saba (7) vitawasili Aprili, 2024.” Imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa TRC itaanza kupokea Seti ya kwanza kati ya 10 za treni za Kisasa (EMU) mwezi Machi 2024 na Mei seti 2, Juni seti 2, Julai seti 2, Septemba seti mbili na seti ya mwisho mwezi Oktoba 2024.

“Vichwa vilivyopokelewa, kiutendaji vina mwendokasiwa kilomita 160 kwa saa. Mabehewa 27 katika madaraja ya uchumi na biashara. Daraja la biashara ‘Business class’ ni mabehewa 13, kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 45 na mabehewa ya daraja la Uchumi ‘Economy class’ ni 14,kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 78 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kumuwezesha abiria kusafiri kwa amani na salama,”

“Shirika la Reli Tanzania linaendelea kupokea kwa awamu vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR). Zoezi la majaribio ya vitendea kazi linaendelea kwa mujibu wa mkataba iii kuhakikisha vinaendana na mifumo ya miundombinu iliyojengwa nchini kabla ya kuanza uendeshajiwa kibiashara.” Imeeleza taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button