Serikali yapoteza sh trilioni 15
SERIKALI imepoteza mapato ya sh trilioni 15 kutokana na kesi za kikodi zilizopo katika mahakama zake za Trab na Trat.
Taarifa ya kamati ya kudumu ya bajeti iliyowasilishwa bungeni imeonyesha kuwa zaidi ya kiasi hicho cha fedha hakijakusanywa katika mwaka wa fedha ulioishia Aprili 23.
Akichangia hotuba ya bajeti kuu, mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema kuwa fedha hizo hazijakusanywa kutokana na usimamizi mbovu.
“Hatujakusanya zaidi ya sh trilioni 15 kwa sababu ya usimamizi mbovu, imeripotiwa hapa hadi kufikia Aprili 23 hatujakusanya fedha ambazo zimeshikiliwa kikodi, zaidi ya sh trilioni 7.35 kesi hizi zipo kwenye mahakama ya kikodi trab na trat.
“Mwaka mzima umeisha tumeshindwaje kukusanya hizi fedha? Kuna changamoto gani?ukiangalia uwezo wa TRA kushinda kesi ni asilimia 81 kwa hiyo kwenye mashauri hayo tunauwezo wa kukusanya trilioni sh trilioni 6. Lakini tatizo ni nini tunashindwa kukusanya?
“Tunaingia kwenye mikopo, kuharass wananchi kuwawekea kodi ambazo hazina sababu za msingi.”Amesema