Serikali yasaini mkataba ujenzi wa MV Magogoni

SERIKALI imesaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni wenye thamani ya Sh bilioni 7.5 ambazo ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Akizungumza katika viwanja vya kivukoni jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema, ukarabati wa kivuko hicho ni juhudi na mikakati ya serikali katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji.

Profesa Mbarawa amesema kuwa miradi mitano ya ujenzi wa vivuko vingine vipya na miradi 16 ya ukarabati wa vivuko unaendela baada ya kusainiwa kwa mikataba yake ambayo hadi kukamilika kwa miradi hiyo itagharimu Sh bilioni 60.7.

Ametoa wito kwa watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kusimamia vema ukarabati wa kivuko hicho utakaofanyika Mombasa nchini Kenya chini ya kampuni ya African Marine and General Engineering Company Ltd kwa muda wa miezi mitano.

Kivuko cha MV Magogoni kilijengwa mwaka 2008, kina uwezo wa kubeba abiria elfu mbili na tani 500 za mizigo yakiwemo magari madogo 60 kwa wakati mmoja.

Habari Zifananazo

Back to top button