Serikali yasisitiza mambo mazuri kwa wajasiriamali

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wajasiriamali ya kuwezesha kupata mikopo na maeneo ya biashara, ili shughuli zao ziwe na tija katika kukuza uchumi.

Amesema hayo akifunga maonesho ya sita ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyomalizika jana mjini Kigoma katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye.

Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye, akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya mifuko na program za uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyokuwa yakifanyika mjini Kigoma(Picha zote na Fadhil Abdallah).

Alibainisha kuwa  shughuli za wajasiriamali zina mchango mkubwa katika kukuza kipato chao kupitia vikundi vyao, mtu mmoja mmoja katika kukuza ajira sambamba na kukuza uchumi wa nchi.

Alisema kuwa kupitia mifuko 72 inayotoa ruzuku, mikopo na huduma mbalimbali, serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri na wezeshi wajasiriamali hao, ikiwemo kuwaunganisha na mifuko na taasisi zinazotoa mikopo, elimu, ithibati ya bidhaa, urasimishaji wa bidhaa, elimu ya kuandaa wazo na mpango wa  biashara.

Ofisa Miradi kutoka Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF), Yohanes Nchimbi akizungumza katika kufunga maonesho.

Awali Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC),Beng’I Issa, alisema kuwa maonesho ya Mifuko na Program za uwezeshaji wananchi kiuchumi zimekuwa na tija kubwa kwa kusogeza huduma kwa wananchi, ili kutembelea mabanda ya taasisi zinazoshiriki na kupata taarifa mbalimbali na

Naye Ofisa Usajili wa Biashara na Leseni kutoka (BRELA), Stanislaus Kigosi alisema kuwa kumekuwa na changamoto katika taratibu za usajili wanazopata watu mbalimbali, hivyo ushiriki wao kwenye maonesho mbalimbali yanasaidia kupata watu wengi ambao wanafika kwenye banda lao na kutatua changamoto hiyo.

Ofisa Usajili wa leseni na biashara BRELA Stanislau Kigosi, akizungumza katika maonesho hayo.

Alisema kuwa pia wamekuwa wakitumia maonesho kupita kwenye mabanda ambayo yana washiriki kutoka mikoa mbalimbali, ambapo wanakutana nao na kuwaelewesha umuhimu wa kusajili majina ya biashara zao na taratibu nyingine ili kuwawezesha kukidhi vigezo vya biashara za kuvuka mpaka.

Habari Zifananazo

Back to top button