Serikali yasitisha shughuli za kibinadamu Mto Ruaha Mkuu ukikauka

Waziri Selemani Jafo na ujumbe wake walipokagua Mto Ruaha Mkuu

SERIKALI imesitisha shughuli zote za kibinadamu katika Mto Ruaha Mkuu baada ya mto huo kukauka kutokana na ukataji miti hovyo, kilimo pamoja na ufugaji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk Selemani Jafo ametoa agizo hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisema uharibifu huo umeathiri shughuli za kiuchumi nchini na umekua sehemu ya upungufu wa maji na umeme.

Dk. Jafo ameagiza bodi za bonde za maji na Baraza la Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira kusimamia vyanzo vya maji kwa wale waliochepusha na wale wanaotumia maji kwa mujibu wa vibali kuangalia suala hilo.

Advertisement

“Kwa kipindi hiki wanyama wakiwemo viboko, Mamba na aina mbalimbali za samaki wapo katika hali mbaya hivyo tuombe mvua zinyeshe kwa kipindi kifupi ili kuwaokoa wanyama hao waendelee kuishi vinginevyo watakufa.

“Mto Ruaha umekauka kabisa tulikuwa tukipita na helikopta kule juu mto umekauka kabisa mto huu hauna maji kabisa yanayotiririka hata ukienda Ihefu hali ni mbaya sana inaenda sambamba na kuathiri sekta nyingine

mfano mzuri sekta ya nishati mimi naamini kiwango cha umeme kinachozalishwa na maji leo hii inawezekana ukienda Mtera naamini kiwango cha umeme kinachozalishwa katika mabwawa haya hali imekuwa ni mbaya sana,” amesema Dk. Jafo

Kupitia Sheria ya Maji ya mwaka 2022, serikali imewataka wakulima kuacha mara moja kulima na kuchepusha maji ya mto Ruaha kinyume na taratibu huku akiwataka kuondoka haraka na kuiagiza mamlaka ya bonde kusimamia sheria hiyo

Kwa upande wake Waziri wa Utalii Balozi Dk. Pindi Chana amesema kuwa wananchi wanatakiwa kushikamana ili kulinda na kutunza maliasili zilizopo pamoja na vyanzo vya maji.

“Wote tulioingia hapa tumeshuhudia kwamba Mto Ruaha Mkuu (GREAT RUAHA) umeanza kukauka nitumie nafasi hii kuutangazia umma na watanzania wenzangu jukumu ni kutunza na kuendeleza maliasili kwa hiyo nawaombeni sana tushirikiane na kuendeleza hifadhi zetu na kuna vyanzo vya maji mengi sana vitasaidia idadi yetu kwa sensa ya mwaka huu maji haya pia yanasaidia hifadhi zetu”

Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) William Mwakilema alisema ukame wa Mto Ruaha ni hatari kwa wanyama na hii ni kutokana bonde la Usangu/Ihefu kuendelea kwa shughuli za kilimo za kuzuia maji kwenye mto Ruaha.

Mwakilema amesema jitihada mbalimbali zinafanyika za kuweza Mto Ruaha kuwa na maji kwa vipindi vyote kutokana na mto huo kuwa na tegemeo kwa Taifa.

“Kipindi hiki ambacho mto umekauka ni kipindi kigumu kwa sababu wanyama wanataabika kupata maji wanyama kupata chakula maeneo ya kupumzika siyo mazuri lakini pia tunaona sisi ambao ni wasimamizi tunawakati mgumu pia kuangalia cha kufanya hali ya mto ruaha sio nzuri na jitihada mbalimbali zinapaswa kufanywa ili kuhakikisha huu mtoto unatirirsha maji vinginevyo uhai wa mto huu utakuwa mashakani “alisema Mwakilema

Kabla ya mkutano huo umechukua masaa matatu ya viongozi kujadiliana kutokana na hali waliokuta katika mto Ruaha ukiwa umekauka.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *