Serikali yasitisha uchimbaji tanzanite Kitalu B

WIZARA ya Madini imesitisha shughuli za uchimbaji madini ya tanzanite katika mgodi wa Gem & Rock Venture uliopo kitalu B Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Inadaiwa kuwa mgodi huo ulikaidi amri ya kusitisha shughuli za uchimbaji  ulipolalamikiwa na kampuni ya Franone inayochimba katika kitalu C kwa kushirikiana na serikali kama mbia.

Hivi karibuni ilidaiwa kuwa wafanyakazi 30 wa Kampuni ya Gem & Rock Venture walivamia mgodi wa Kitalu C na kuchimba madini ya tanzanite.

Ilidaiwa kuwa wafanyakazi hayo walipora madini hayo lakini uongozi wa kampuni hiyo ulipinga na kusema kuwa wao ndio wameporwa tanzanite yenye uzito wa kilo sita.

Ofisa Madini Mfawidhi Mkoa Mkoa wa Manyara, Mernad Msengi alisema watalaamu wa Chuo Cha Madini Dodoma wanatarajiwa kuwasili Arusha leo kupima madini yaliyokamatwa katika vurugu kama ni mali ya kitalu B au C ili kumaliza utata huo.

Msengi alisema sakata la vurugu zilizoibuka ndani ya Mgodi wa Tanzanite wa Kitalu C lipo katika mikono ya dola hivyo wafanyakazi katika maeneo hayo wasubiri uchunguzi.

Msengi alisema kwa njia ya simu kuwa jukumu la wataalamu kutoka Dodoma ni kuangalia kama madini yaliyohifadhiwa na ofisi yake kama kweli yanatoka kitalu B au C.

 

Habari Zifananazo

Back to top button